Wolper- Mapenzi na Ali Kiba Yalikuwa Bora Zaidi


Staa wa filamu za Bongo Movie na mjasiriamali Jacqueline Wolper ameibuka na kudai hakuna mwanaume ambaye alikuwa mpenzi bora kwake kama ilivyokuwa kwa staa wa Bongo fleva Ali Kiba.
Wolper ambaye siku za nyuma amewahi kukiri kuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi kwa muda mrefu na Ali Kiba ingawa hawakuyaweka hadharani na kujulikana na mashabiki.
Kwenye mahojiano aliyiwahi kufanya na East Africa Television, Wolper amefunguka na kuongea haya:
Katika Mahusiano yangu yote ambayo nimewahi kuwa nayo, ambayo naweza kuyapa namba moja na yalikuwa mazuri na ni the best ni yale nilipokuwa na Ali Kiba. Lakini sio kwamba namiss hapana ila tu ninasema yalikuwa Mahusiano bora niliyowahi kuwa nayo”.
Mbali na Ali Kiba, Wolper ameshawahi kuwa Kwenye Mahusiano na mastaa wengine kama Harmonize, Juma Jux na wengineo.
The post Wolper- Mapenzi na Ali Kiba Yalikuwa Bora Zaidi appeared first on Ghafla!Tanzania.

Comments

Popular posts from this blog

Hizi hapa SMS kali mpya Za Mapenzi

SMS Ambayo Itamfanya Mwanamke Akutamani

MESEJI NZURI ZA KUMTUMIA MPENZI WAKO